Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wammwagia minoti Waitara kisa mkataba wa Bandari

IMG 20230610 WA0009 Wabunge wammwagia minoti Waitara kisa mkataba wa Bandari

Sat, 10 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya Wabunge wameinuka na kumchangia fedha Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara wakati akichangia mjadala wa Azimio la Serikali kuomba Bunge kuridhia mkataba baina ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii wa Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania.

Katika Mchango wake Waitara amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kufanya kazi na imekuwa hivyo na amekuwa kiongozi ambaye anapenda uwazi na kutaka akosolewe kwa hoja.

“Tuhuma za kiongozi yule kusema Rais ni Mzanzibari na Waziri (Prof. Makame Mbarawa) ni Mpemba wanataka kuuza Bandari ya Dar es Salaam, Mh. Mbowe amemkosea sana Rais Samia na Watanzania.

“Mh. Mbowe anapaswa kumuomba radhi Mh. Rais. … Kitendo hiki lazima tukichukulie hatua. Ukimsema Rais wa nchi umesema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na viongozi na wafuasi wa CCM hatuwezi kukaa kimya kwa mambo kama haya. Tunataka watu walete hoja za msingi, watukosoe na Rais ameruhusu kukosolewa kwa hoja.

“Nataka niwaombe wananchi na wanaCCM hii ni dalili nzuri watu hawa hawawezi kuongoza nchi na Mh. Rais ajiandae 2025 njia ipo wazi abeb msalaba huu na sisi tunamwamini wanawake wananweza na chenji inabaki.

Tunataka tumpe heshima Rais wetu. Watanzania wanamwamini na Spika wewe ni Wakili msomi huwezi kuruhusu mkataba wa hovyo … haiwezekani. Wasione kwamba wabunge wa CCM hatujui, tunajua sana. Na Mh. Rais atuache kidogo tushughulike na watu hawa,” amesema Waitara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: