Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wacharuka posho za madiwani

Images (1) Waitara.jpeg Mwita Waitara.

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sakata la posho za madiwani na wenyeviti wa vijiji limeibuka kwa mara nyingine bungeni leo Ijumaa Septemba 8, 2023 ambapo wabunge wamehoji ni lini Serikali itawaongeza posho madiwani na wenyeviti wa vijiji.

Mbunge wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara ndiye aliyeibua swali la msingi baada ya kuhoji ni lini madiwani na wenyeviti wa vijiji wataongezwa posho.

Wabunge wengine waliouliza maswali ya nyongeza waliohoji kuhusiana na suala la posho za madiwani na wenyeviti wa CCM ni Festo Sanga (Makete), Rashid Shangazi (Mlalo) na Neema Lugangira (Viti Maalum).

Akijibu Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk Festo Dudange amesema Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na madiwani na wenyeviti wa vijiji katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kila halmashauri inatakiwa kuweka utaratibu wa kuwalipa posho, madiwani na wenyeviti wa mitaa na vijiji kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ya halmashauri.

“Kutokana na changamoto za mapato kwenye halmashauri nyingi nchini, Serikali ilianza kutenga bajeti katika mwaka wa fedha 2021/22 kwa ajili ya kulipa posho za waheshimiwa madiwani pamoja na wenyeviti wa vijiji,”amesema.

Amesema katika mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imetenga kiasi cha Sh22.5 bilioni kwa ajili ya kulipa posho za madiwani na Wenyeviti wa vijiji katika halmashauri 168,”amesema.

Amesema Serikali inaendelea kuzijengea uwezo mamlaka za serikali za mitaa ili ziweze kubuni na kuimarisha vyanzo vya mapato pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha kwa kutumia mifumo ya kieletroniki ya kukusanya na kutumia fedha katika kutekeleza miradi ya maendeleo pamoja na matumizi mengineyo ili kuongeza uwezo wa malipo kwa viongozi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: