Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vilio, Simanzi vyatawala nyumbani kwa Membe (+Video)

Video Archive
Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vilio, Huzuni na Simanzi vimeendelea nyumbani yalipokuwa makazi ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Mwanadiplomasia mbobezi Bernad Membe aliyefariki Leo Jijini Dar Es Salaam katika Hospitali ya Kairuki wakati akipatiwa matibabu.

Viongozi Mbalimbali, Watu Mashuhuri pamoja na Waombolezaji wengine wameendelea kufika Msibani ili kuomboleza Kifo cha Mwanasiasa huyo Mkongwe hapa nchini ambae wakati uhai wake aliweza kushika nyadhifa mbalimbali za Kiuongozi Serikalini.

Kulingana na Taarifa iliyotolewa na Msemaji rasmi wa Familia ya Membe, Shughuli ya Kuupumzisha mwili wake inatarajiwa kufanyika Mei 16 kijijini kwake Rondo-Chiponda mkoani Lindi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live