Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Yatima manusura wa Mv Bukoba awasaka ndugu zake kwa miaka 23

Video Archive
Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Ni miaka 23 sasa imepita Samuel Mv Bukoba (27) ambaye ni mmoja wa manusura wa ajali ya meli ya Mv Bukoba anatafuta ndugu zake bila mafanikio.

Samuel ambaye jina lake la pili la Mv Bukoba alipewa na walezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Mabatini jijini Mwanza alinusurika katika ajali hiyo iliyotokea Mei 21, 1996 baada ya mama yake ambaye hamkumbuki jina kumrusha juu ya mkungu wa ndizi iliyokuwa ikielea juu ya maji pembeni mwa meli iliyokuwa inazama.

Akizungumza jana Mei 21, 2019 wakati wa ibada ya kumbukizi ya ajali hiyo iliyofanyika eneo la makaburi ya Igoma jijini Mwanza, Samuel alisema licha ya kupata misaada ya hali na mali kutoka kwa wasamaria wema tangu aliponusurika, kiu yake kubwa ni kuwafahamu ndugu na asili yake.

“Ni mwaka wa 23 sasa nafanya jitihada kuwatafuta ndugu zangu bila mafanikio. Nimejitahi mimi mwenyewe, walezi wangu pamoja na Serikali lakini hatujafanikiwa,” alisema.

Akifafanua, kijana huyo anasema si kwamba anawatafuta ndugu kwa sababu ya kukosa mahitaji, bali anafanya hivyo kutokana na umuhimu wa kujua asili na chimbuko lake.

Wakati ajali ya Mv Bukoba iliyogharimu maisha ya watu zaidi ya 800, Samuel alikuwa na umri wa miaka minne.

Pia Soma

“Tangu wakati huo, nimelelewa kwenye kituo cha yatima Mabatini ambako wasamaria wema wamekuwa wakijitokeza kunisaidia hadi hapa nilipofikia; nawashukuru wote walionisaidia na wanaoendelea kunisaidia kwa hali na mali. Lakini nitafurahi zaidi siku nikiwajua ndugu zangu,” alisisitiza

Yatima huyo aliiomba Serikali kutumia ajali ya Mv Bukoba kama fundisho la kuongeza ubora na usimamizi wa sheria, kanuni na taratibu za usafirishaji, si tu majini, bali hata angani na nchi kavu.

Kwa habari zaidi soma magazeti ya Mwananchi na The Citizen kesho

Chanzo: mwananchi.co.tz