Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Wanafunzi 58,699 kusubiri ujenzi wa madarasa kuanza kidato cha kwanza

Video Archive
Thu, 5 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Leo Alhamisi Desemba 5, 2019 Serikali ya Tanzania imesema wanafunzi 759,737 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 wataanza kidato cha kwanza mwaka 2020.

Kati yao, 58,699 watalazimika kusubiri kukamilika kwa ujenzi wa madarasa kabla ya Machi  mwaka 2020 ili waweze kuendelea na kidato cha kwanza.

Kati ya wanafunzi watakaokwenda moja kwa moja kidato cha kwanza, 3,145 watajiunga na shule za bweni na 697,893 watajiunga na  shule za sekondari za kata.

Akizungumza leo Alhamisi Desemba 5, 2019 Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo ametaja mikoa ambayo wanafunzi watasubiri ujenzi huo.

Mikoa hiyo na idadi ya wanafunzi kwenye mabano ni  Arusha (4,739), Dar es Salaam (5,808), Iringa (3,480), Kigoma (12,092), Lindi (1,695), Manyara (728) na Mara (9,494), Mbeya (2,216) Pwani (2,918),Rukwa (686), Simiyu (6,616),Songwe (4,684) na Tanga (3,044).

"Wakuu wa mikoa na wilaya ifikapo Februari 29, 2020  nataka madarasa yote yawe yamekamilika na wanafunzi waanze masomo Machi 2, 2020. Makatibu tawala wa mikoa wahakikishe wanasimamia hilo," amesema Jafo.

Jafo amesema Mikoa 13 ambayo wanafunzi wataanza masomo moja kwa moja kutokana na kutokuw ana uhaba wa madarasa ni Dodoma, Geita, Kagera, Katavi, Shinyanga, Singida, Tabora, Kilimanjaro, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe na  Ruvuma.

Chanzo: mwananchi.co.tz