Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Waitara: Nimepiga kura ya ushindi

Video Archive
Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mgombea ubunge wa Ukonga kupitia CCM, Mwita Waitara amesema anashukuru amepiga kura ya ushindi.

Waitara amesema hayo mara baada ya kupiga kura kwenye kituo cha Kerezange kilichopo Kivule asubuhi ya leo Septemba 16, 2018.

Amesema amepigania kwenye kampeni na anaamini kura yake ni ya ushindi.

Akizungumza kuhusu tishio la vurugu, Waitara amesema hakuna vurugu kwa sababu wageni waliokuja wakati wa kampeni wameshaondoka waliobaki ni wenyeji.

"Hili ni jimbo letu sisi mwisho wa siku tumebaki wenyewe wajuaji wameshaondoka, hivyo hakuna vurugu,” amesema Waitara.

"Ukumbuke hili jimbo lina mitaa 70 saba tu ndiyo ya upinzani na 63 ni CCM, unaweza kuona ni kwa jinsi gani hakuwezi kuwa na vurugu hakuna anayeweza kuifanyia vurugu CCM," amesema Waitara.

Akizunguimzia mwitikio mdogo wa wapiga kura asubuhi hii, Waitara amesema ni kwa sababu Jumapili ni siku ya ibada hivyo watu bado wapo makanisani.

"Wanajua kuwa mwisho wa kupiga kura ni saa 10 jioni na sasa ni (ilikuwa saa 4 asubuhi) bado wana saa sita za kupiga kura," amesema Waitara.

Chanzo: mwananchi.co.tz