Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Ulega asema wavuvi nchini Tanzania mbioni kusajiliwa

Video Archive
Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Serikali ya Tanzania imetangaza kuanza kuwasajili wavuvi katika mfumo wa kielektroniki  ili kuepusha vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na baadhi yao katika maeneo yao ya kazi.

Kauli hiyo imetolewa jana Agosti 2, 2019 na naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah ulega wakati akifungua mkutano wa wadau wa vyama vya ushirika uliofanyika katika maabara ya ubora wa mazao ya uvuvi Nyegezi mkoani Mwanza.

Lengo la mkutano huo ilikuwa kujadili sekta ya uvuvi na uhitaji wa ushirika wa wavuvi, kuweka mikakati ya ushirika wa wavuvi wa kanda ya ziwa.

“Sasa tunataka usajili wa wavuvi wote na vyombo vyao uwe wa kielektroniki maana wasio waaminifu wanaleta matatizo.”

“Kwanini leo mvuvi afikie hatua ya kuua ofisa wa Serikali? Tunataka kila aingiaye katika sekta hii ajulikane hivyo lazima kuwe na kanzi data kwa mfumo wa kidigitali,” amesema Ulega.

Ameongeza, “Bado ni aibu kwa sekta hii kubwa na pana mchango wake katika Pato la Taifa kuwa asilimia mbili. Tunataka kuona sekta hii inakuwa na mchango mkubwa kama ilivyo pana.”

Pia Soma

“Watu wanataka rasilimali za ziwa ziishie lakini uvuvi ni kama shughuli nyingine, tunataka urasimishwe, utambulishwe na kuwa kazi ya heshima kama nyingine,  hivyo mkutano huu utengeneze mpango kazi wa wote kusimamia rasilimali za uvuvi na kuwatajirisha wavuvi.”

Naibu Waziri huyo amesema sekta hiyo ikisimamiwa kikamilifu itakuza Pato la Taifa kwa maelezo kuwa kupitia sekta hiyo makusanyo ya Julai , 2019 kitaifa yalikuwa Sh16.4 bilioni na Serikali kupata mrabaha wa Sh1.6 bilioni.

Awali,  mkurugenzi wa uvuvi nchini,  Magesa Bulai  amesema  wavuvi wanaotambulika hivi sasa nchini ni 220,000 na kwamba zaidi ya watu milioni nne wanategemea sekta hiyo kuendesha maisha.

Chanzo: mwananchi.co.tz