Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Ujenzi wa kaburi la Mengi wafikia hatua za mwisho

Video Archive
Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Ujenzi wa kaburi ambalo atakazikwa aliyekuwa mwenyekiti mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi uko katika hatua za mwisho, huku taratibu za mazishi zikiwa zinaendelea.

Mazishi ya Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2 akiwa Dubani, Falme za Kiarabu yatafanyika kesho kijijini kwao Nkuu, Machame mkoani Kilimanjaro.

Wakati Shughuli za ujenzi wa kaburi zikiendelea nyumbani alikozaliwa, baadhi ya vijana wameendelea na shughuli za usafi wa mazingira na kuweka mambo sawa katika eneo hilo ambalo linatarajiwa kupata ugeni mkubwa kwa ajili ya mazishi hayo.

Kaburi la mwenyekiti huyo limepakana na kaburi la mwanaye, Rodney Mutie Mengi aliyefariki mwaka 2005.

Hata hivyo, mamia ya wakazi wa kijiji hicho wamehama kijiji chao na kuhamia kijiji cha Nkweseko kwa ajili yakupokea mwili wa marehemu ambako utahifadhiwa kwa muda hadi kesho.

Kesho mwili wa Mengi aliyezaliwa Mei 29, 1942 utaaagwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Moshi Mjini na kisha kupelekwa kijijini kwao Nkuu kwa ajili ya mazishi.

Habari zinazohusiana na hii



Chanzo: mwananchi.co.tz