Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Udom wazungumzia matokeo ya wanafunzi 8,500 kuzuiwa

Video Archive
Mon, 9 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) nchini Tanzania kimezuia matokeo na wanachuo zaidi ya 8,500 kutokana sababu mbalimbali ikiwamo suala la ada.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Septemba 9, 2019 chuoni hapo, Ofisa Uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazary amesema uamuzi wa kuzuia  matokeo hayo ni wa kikao cha seneti ya chuo kilichofanyika Septemba 6, 2019.

Amesema wapo ambao hawajalipa ada, wengine hawajamalizia ada.

"Wanafunzi ambao matokeo yao yamezuiliwa ni wa shahada ya awali 8,329 na shahada ya juu 418 kutoka ‘collage’ zote saba za chuo cha Udom.”

“Wanafunzi hawajakamisha taratibu za chuo ikiwemo masuala ya kulipa ada,” amesema Baltazary

Hata hivyo, amesema wanafunzi hao hakuna atakayefukuzwa chuo bali hataruhusiwa kuona matokeo yake hadi alipe ada ili aruhusiwe kurudia kufanya mitihani atakayokuwa amefeli.

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz