Dar es Salaam. Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema serikali haina mpango wa kuficha kuhusu ugonjwa wa ebola, kusisitiza kuwa ugonjwa huo haupo nchini.
Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 3, 2019, Ummy amesema kuna tishio la ugonjwa huo kutokana na mwingiliano kati ya Tanzania na nchi ya nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DCR) ambako kuna ugonjwa huo.
“Huu sio ugonjwa wa kufichwa. Serikali tunatambua madhara ya kuficha ugonjwa huu na tunafahamu taratibu za kutoa taarifa za magonjwa ya mlipuko,” amesema Ummy.
Ummy amesema kuna nia ovu za kueneza taarifa hasi dhidi ya Tanzania hivyo wananchi wapuuze habari hizo.
“Wananchi tuwe watulivu na kushikamana kwa pamoja, tishio la ugonjwa huu lipo na akitokea mtu atakayethibitishwa kuwa na ugonjwa huo tutazingatia miongozo na kanuni katika kutoa taarifa,” amesema.
Pia Soma
- Viongozi CUF wamlalamikia Lipumba uchaguzi uliopita Ukawa iliwavuruga
- Wananchi wachangishana, wajenga vyumba 1510 vya madarasa
- Hakimu ahoji mashahidi kutopelekwa mahakamani kesi ya Halima Mdee