Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Serikali ya Tanzania yajivunia kuimarika kiuchumi

Video Archive
Fri, 7 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema licha ya kuendelea kwa mdororo wa uchumi lakini Tanzania imeendelea kufanya vizuri kibiashara huku urari wa biashara ukiendelea kuimarika.

Hayo yamesemwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Ijumaa Juni 7, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam katika kikao chake na wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini kilichohudhuriwa pia na watendaji mbalimbali wa Serikali.

Amesema mwaka 2018 Tanzania iliuza kwenye soko la Afrika Mashariki bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani 447.5 milioni ikilinganishwa na dola za kimarekani 349.6 milioni mwaka 2017.

“Bidhaa tulizoagiza kutoka nchi za Afrika Mashariki mwaka 2018 zilikuwa za dola za kimarekani 302.93 milioni ikilinganishwa na dola za marekani 220.4 mwaka 2017.”

“Soko la (Jumuia ya Ushirikiano na Maendeleo Kusini mwa Afrika) SADC mwaka 2018 Tanzania iliuza bidhaa zenye thamani ya dola za Marekani 999.34 milioni ukilinganisha na dola za Marekani 877.8 milioni mwaka 2017,” amesema Magufuli

Amesema, “Bidhaa zilizonunuliwa kutoka SADC zilikuwa na thamani ya dola za kimarekani 604.3 milioni ikilinganishwa dola za marekani milioni 600.6 mwaka 2017.”

Habari zinazohusiana na hii

Pia amesema tangu Serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani Novemba 5, 2019 jumla ya kampuni na biashara mpya 74,715 zimesajiliwa huku kati yake 30,716 zikisajiliwa na Brela.

Magufuli amesema majina ya bishara 54,657 yamesajiliwa huku leseni za bishara zilizotolewa na mamlaka za serikali za mitaa 655,340 huku viwanda vipya 3,500 vikijengwa

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz