Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Profesa Assad amshauri Kichere kuhusu kuwafanyia mabadiliko ya watumishi wa taasisi hiyo.

Video Archive
Fri, 8 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Siku moja baada Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere kuapishwa, CAG aliyemaliza muda wake, Profesa Mussa Assad Juma amempa ushauri wa namna ya kuendesha ofisi hiyo.

Profesa Assad amemueleza kuwa ni vyema akawajengea uwezo watumishi waliopo kuliko kuwafanyia mabadiliko kwa haraka kwa sababu hatua hiyo inaweza kuharibu utendaji wa taasisi.

“Taasisi haitakiwi kufanyiwa mabadiliko ya haraka muhimu ni kuwajengea uwezo waliopo, kinyume na hapo unaweza kuharibu taswira.”

“Huwa naamini changes (mabadiliko) zinaweza kutokea ila zitokee katika namna ambayo zimepangwa vizuri, si mwaminifu katika mfumo wa kutoa watu wote na kuweka new team usually lazima kutakuwa na mkanganyiko and can be very expensive kwa institutions kama hizi ambazo mtu anajifunza kwa miaka mingi.

“Kufikia level ya DAG lazima amefanya kazi na amekaa kwenye ofisi miaka 10 hadi 15, kwa hiyo experience yake ni muhimu kuihamishia kwa mtu mwingine, ukifanya immediate changes unaweza kupoteza ile instution memory,” amesema Profesa Assad

Jana wakati wa hafla ya kumwapisha Kichere, Rais John Magufuli alimtaka akaisimamie kikamilifu ofisi hiyo na kuisafisha.

“Kasimamie hiyo ofisi kuna baadhi ya watendaji wako wanapokwenda kukagua kwenye balozi wanaomba fedha, sasa nenda kawachambue. Ofisi ya CAG sio clean (safi) kama mnavyofikiria, sasa nenda kachambue ukapange positions (nafasi) za watu wako, ili mauchafu haya ukayasafishe.

“Nenda kafanye kazi, mwenzako aliyekuwapo amemaliza muda wake leo, kwa hiyo kesho uende ofisini ukaanze kazi, kayatoe mauchafu yote utakayoyakuta mengine waulize Wizara ya Fedha wanayafahamu,” alisema Rais Magufuli.

Chanzo: mwananchi.co.tz