Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Ponda adai Magufuli amechelewa kumtumbua Lugola

Video Archive
Fri, 24 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda amedai Rais John Magufuli alitakiwa kutengua uteuzi wa Kangi Lugola tangu Aprili, 2019.

Lugola aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani uteuzi wake ulitenguliwa jana Alhamisi Januari 23, 2020 na Rais John Magufuli na nafasi yake kuchukuliwa na George Simbachawene ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Januari 24, 2020 Ponda amesema Lugola alitakiwa kuondolewa mapema kwa madai kuwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilitaja ubadhirifu uliofanyika katika wizara ya Mambo ya Ndani.

“Jambo linakuwa zuri linapofanyika ndani ya wakati kwa sababu suala la ubadhirifu ndani ya wizara lilielezwa vizuri zaidi na CAG baada ya kutoa uchambuzi wa kina na kutoa ufafanuzi jinsi ubadhirifu ulivyofanyika ndani ya wizara na kiasi kikubwa cha pesa hakijulikani kilipo.”

“Hata utundu uliokuwa ukifanyika katika kughushi baadhi ya vitu lakini Lugola aliendelea kutamba na CAG ndiyo akaanza kushambuliwa na Lugola mwenyewe akiwa mmoja ya waliorusha mashambulizi,” amesema Ponda

Ripoti ya CAG

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Aliyekuwa mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad alibaini ubadhirifu katika Jeshi la Polisi huku Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited ikitajwa kwa mara nyingine kuhusika.

Profesa Assad amesema ukaguzi umebaini kuwa mahitaji ya kitaalam kutoka idara inayotumia mfumo wa Utambuzi wa Alama za Vidole (AFIS) ulibaini kuwa mahitaji ya kitaalam kutoka idara inayotumia mfumo huo hayakuzingatiwa wakati wa kuthamini na kutoa zabuni.

“Malipo ya Sh3.30 bilioni yalifanyika kwa mzabuni kwa ajili ya huduma ya matengenezo na msaada wa kitaalam wa Mfumo wa Utambuzi wa Alama za Vidole,” amesema.

Amesema huduma hiyo ilipangwa kufanyika mikoa nane ya kipolisi ya Temeke, Mwanza, Simiyu, Tabora, Kigoma, Geita na Kinondoni lakini Jeshi la Polisi lilishindwa kuthibitisha kuwa matengenezo hayo na msaada wa kitaalam ulifanyika.

Profesa Assad amesema vifaa vya utambuzi wa alama za vidole vyenye thamani ya Sh1.73bilioni havikufungwa kwenye magereza 35 kama ilivyoainishwa badala yake vilihifadhiwa katika ofisi ya upelelezi Makuu ya Jeshi la Polisi.

 “Malipo ya Sh604.39 milioni kwa ajili ya mafunzo kwa wataalamu 30 hayakufanyika,”amesema.

Amesema Jeshi la Polisi lilishindwa kuionyesha timu yake ya ukaguzi zilipo monita 58 za kompyuta aina ya Dell zenye thamani ya Sh159.16 milioni zilizopelekwa kwenye kitengo cha uchunguzi wa kisayansi cha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi (Forensic).

Pia amesema monita 213 za kompyuta aina Dell zilizolipiwa Sh195.22milioni kwa mzabuni Lugumi Enterprises Limited lakini mzabuni hakuzileta.

Aidha, amesema ukaguzi wa ununuzi wa sare za askari polisi, umebaini jeshi hilo lililipa Sh16.66 bilioni bila kuwapo na ushahidi wa uagizaji na upokeaji wa sare za askari polisi wa boharia mkuu wa Jeshi la Polisi.

“Pia nilibaini maoni ya kisheria ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanayohusu uwasilishaji wa kiapo cha nguvu ya kisheria (Power of Attorney) na leseni halali ya biashara hayakuzingatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara wa Mambo ya Ndani wakati wa kusaini mkataba uliohusu ununuzi wa sare za askari polisi,” amesema.

Profesa Assad amesema anapendekeza Jeshi la Polisi lihakikishe kuwa vifaa vya utambuzi wa alama za vidole vinafungwa katika maeneo husika na kuanza kutumika ilivyokusudiwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz