Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mwili wa Kibonde wawasili nyumbani

Video Archive
Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde, umewasili wakati huu hapa nyumbani kwa wazazi wake, maeneo ya Mbezi Africana jijini Dar es Salaam.

Kibonde alifariki Machi 6, 2019 alipokuwa akiwahishwa Hospitali ya Bugando Mwanza baada ya hali yake kubadilika ghafla alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Uhuru jijini Mwanza.

Baada ya taratibu zote za kuaga na ibada, msafara utaondoka hapa nyumbani milango ya saa 9 kwenda kumlaza kwenye nyumba yake ya milele, katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Kibonde alikuwa muongozaji wa shughuli (MC) kwenye msiba wa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba aliyezikwa Machi 4, 2019, alianza kujihisi vibaya mara baada ya maziko hayo yaliyofanyika Bukoba mkoani Kagera.



Chanzo: mwananchi.co.tz