Dar es Salaam. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametaja sababu tatu za kuipenda Tanzania mara baada ya kuwasili wilayani Chato Mkoa wa Geita katika ziara yake binafsi ya siku moja.
Mara baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, John Magufuli, leo Jumamosi Julai 13, 2019 kiongozi mkuu huyo wa Uganda amesema jambo la kwanza ni undugu wa wananchi wanaoishi katika maziwa makubwa.
“Sababu ya pili ni uwepo wa njia muhimu tangu enzi za ukoloni ambazo zimeunganisha maeneo ya Pwani hadi Uganda. Tena nitamuomba Rais Magufuli anipeleke eneo la Bwanga jijini Mwanza lililopo kilometa 30 kutoka Chato,” amesema Museveni.
Amesema sababu ya tatu ni mapambano yaliyofanywa na Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania kutetea uhuru wa nchi mbalimbali ikiwemo Uganda na zilizopo Kusini mwa Afrika.
“Kama namna Waislamu wanakwenda Macca na Wakristo Roma sisi wapigania uhuru tunakwenda Dar es Salaam,” amesema Museveni.
Pia Soma
- Trump atangaza kiama kwa wahamiaji Marekani
- LIVE :Museveni awasili Chato
- Wawekezaji waonyeshwa maeneo ya uwekezaji mkoani Mtwara