Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mbunge CCM atunishiana misuli na Spika, aitwa kamati za maadili

Video Archive
Thu, 16 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Spika wa bunge Job Ndugai amemsimamisha kwa muda uwakilishi wa mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele katika bunge la Afrika (PAP) hadi taarifa rasmi zitakapotolewa.

Kutokana na hilo, amemtaka mbunge huyo kurudi haraka nchini ambako pia atafikia mikononi mwa kamati za maadili za Bunge na chama chake (CCM).

Katika taarifa yake bungeni leo Alhamisi Mei 16,2019, Spika wa bunge Job Ndugai amesema mbunge huyo amekuwa akifanya mambo ya hovyo na kugonganisha mihimili.

"Amefanya mambo ya utovu wa nidhamu huko  na taarifa tumezipata na hata kwenye mitandao imeonekana, sasa tumemtaka arudi lakini amegoma hivyo nimemwandikia barua Raid wa PAP kusimamisha kwa muda ubunge wa mheshimiwa huyu had I tutakapotoa taarifa nyingine," amesema Ndugai.

Akizungumzia kugoma kurudi kwa mbunge huyo, anasema alimtaka arudi toka jana lakini bado aliendelea kumgomea akisema Spika hawezi kumuita kwa kuwa ana kibali cha Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa Ndugai, hata hapa nchini mbunge huyo amekuwa na tabia zisizokuwa za kibunge ambazo zinalifanya bunge lisitambue msimamo wake ni upi.

Pia Soma

Spika Ndugai ameeleza pia kuwa bunge limekaguliwa kama zilivyokaguliwa kampuni zingine hivyo hakuna aliye juu au anayeweza kujikagua.

Amesema taarifa ya ukaguzi huo ambao ukifanywa na kampuni ya EK Mongosho & Company itapelekwa kamati ya PAC kwa hatua zaidi.

Chanzo: mwananchi.co.tz