Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa hati ya dharura, leo, Jumatatu, Agosti 23, 2021 kusomewa mashatka yanayowakabili. Viongozi wa vyama vya siasa wamehudhuria katika kesi hiyo huku ulinzi ukiwa umeimarishwa.
Ijumaa, tarehe 13 Agosti 2021, mawakili upande wa utetezi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba. Akiwasilisha ombi hilo, Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala, alidai matamshi hayo ambayo hakuyataja, yataathiri mwenendo wa kesi hiyo.
Alidai, wateja wake wanayaona matamshi hayo kama hukumu, kuwa yanaingilia moja kwa moja uhuru wa mahakama, ambapo siyo mahakama ya Kisutu tu bali hata mahakama itakayoenda kusikiliza shauri hilo la ugaidi linalomkabili Mbowe na wenzake, hivyo hawana imani kama mashtaka yao yataendeshwa kwa uhuru mahakamani ambapo ilikuwa isikilizwe tena Agosti 27, lakini ameletwa leo kwa hati ya dharura.
Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita yakiweno ya kufadhili vitendo vya ugaidi na kukusanya pesa kwa ajili ya kufanya vitendo vya kigaidi, katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 63/2020.
Mashtaka mengine ni kula njama za kutenda makosa, kukutwa na silaha aina ya bastola, risasi pamoja na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kinyume cha sheria. Mbali na Mbowe, ambaye ni mshtakiwa wanne katika kesi hiyo, wengine ni Halfan Hassan, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.