Dar es Salaam. Baraza la Taifa la Mitihani nchini Tanzania (Necta) jana Jumanne Oktoba 15, 2019 lilitangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 ambapo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu.
Mwananchi linakuchambulia mambo manane yaliyojitokeza katika matokeo hayo ambayo yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78 lakini ufaulu katika somo la Kiingereza bado mdogo likilinganishwa na masomo mengine.
Kiwango cha ufaulu
Kiwango cha ufaulu kimeongezeka kutoka asilimia 78.38 mwaka 2018 hadi asilimia 81.50. Ongezeko hilo ni la asilimia 3.78 ambapo jumla ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo ni 933,369.
MATOKEO YOTE BONYEZA HAPA
Wafutiwa matokeo
Pia Soma
- Aliyetajwa na Magufuli kuiba Sh7 milioni kwa dakika aachiwa huru
- Magufuli ataja sababu kutumia magari ziara yake mkoani Lindi
- Dk Ndugulile ataja sababu sekta ya afya Wilaya ya Tunduru kuimarika
- Madaktari Zimbambwe wapuuza amri ya mahakama, waendelea kugoma
Mikoa Kanda ya Ziwa yang’ara
Kanda ya Ziwa imeongoza kwa kutoa shule kumi bora kitaifa huku shule ya Graiyaki iliyopo wilayani Serengeti ikibeba bendera ya ufaulu katika kanda hiyo. Mwaka 2018 kanda ya ziwa ilitoa shule nane katika shule 10 bora kitaifa.
Dar na ufaulu
Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa kupata ufaulu wa asilimia 93.28 ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha kisha Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani. Hata hivyo, kwa ngazi ya halmashauri Jiji la Arusha limeongoza likifuatiwa na Kinondoni.
MATOKEO YOTE BONYEZA HAPA
Ufaulu Hesabu, Kiingereza washuka
Ufaulu wa masomo ya Hesabu na Kiingereza umeshuka kwa asilimia 1.05 ikilinganishwa na mwaka 2018. Mwaka 2019 watahiniwa wameonekana kufaulu zaidi katika somo la Kiswahili kama ilivyokuwa mwaka 2018 ambapo ufaulu wake ni asilimia 87.25.
Shule 10 zilizofanya vizuri
Shule 10 zilizofanya vizuri kitaifa ni Graiyaki (Mara), Twibhoki (Mara), Kemebos (Kagera), Little Treasures (Shinyanga), Musabe (Mwanza), Tulele (Mwanza), Kwema Morden (Shinyanga), Peaceland (Mwanza), Mugini (Mwanza) na Rocken Hill (Shinyanga).
Wanafunzi 10 bora wavulana
Wanafunzi 10 wavulana na shule kwenye mabano ni Francis Gwai (Paradise), Victor Godfrey (Graiyaki), Aziz Yassin (Graiyaki), Goldie Hhayuma (Graiyaki), Daniel Ngassa Daniel (Little Treasures), Hilary Nassor (Peaceland), Mbelele Dalali (Kwema Modern), Derick Lema (Musabe), Athanas Sekuro (Paradise) na Aron Mabuga (Kwema Modern).
MATOKEO YOTE BONYEZA HAPA
Wanafunzi 10 bora wasichana
Kwa upande wa wasichana wanafunzi 10 bora ni Grace Manga (Graiyaki), Loi Kitundu (Mbezi), Nyanswi Richard (Graiyaki), Neema Mushi (Graiyaki), Maryleocadia Nkuba (Peaceland), Heavenlight Hhayuma (Twibhoki), Roseleader Steven (Twibhoki), Pilly Zacharia (God’s Bridge), Scholastica Shelembi (Little Treasures) na Suzan Fridoline (Little Treasures).