Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mama Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanaye

Video Archive
Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Verdiana Mjwahuzi (81) ambaye ni mama wa mwandishi wa habari, Erick Kabendera amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumsamehe mwanaye.

Akizungumza kwa huzuni leo Ijumaa Desemba 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Verdiana amesema Kabendera ni mwanaye pekee anayemsaidia katika matibabu.

Kabendera anakabiliwa  na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole,  alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.

Verdiana amesema kati ya watoto wake wanane, Kabendera ni wa saba kuzaliwa na ndio alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza.

">"Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma.”

"Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake,” amesema.

Amesema mwanaye alijitahidi kuitunza familia yake, yeye na ndugu zake wengine na kusisitiza kuwa ndio mhimili wa familia.

"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," amesema mama huyo huku akibubujikwa machozi.

Ameongeza, “kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.

"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu. Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi."

Chanzo: mwananchi.co.tz