Dar es Salaam. Makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Jumamosi Septemba 15, 2018 yameshindikana kuuzwa kwa mara ya nne mfululizo.
Makontena hayo yameshindikana kuuzwa katika mnada uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Soma zaidi:
:VIDEO: Makontena ya Makonda kaa la moto, yakosa mnunuzi kwa mara ya tatu
:TRA yakataa kuuza bidhaa mojamoja ndani ya makontena ya Makonda
Akizungumza kwenye mnada huo, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kevela amesema mnada huo umeendeshwa lakini mnunuzi hajapatikana.
Kevela amesema hadi sasa bei zinazofikiwa na wateja hazijafikia malengo waliyowekewa.
Soma zaidi.
:Mbunge ampongeza Waziri Mpango kwa kumshughulikia Makonda
:Msimamo wa Dk Mpango dhidi ya Makonda mjadala
“Ni kweli wateja wanakuja na bei lakini hazijafikia zile ambazo TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) wametuwekea kama kodi yao," amesema.
Amesema wao kama madalali wataendelea kufanya utafiti wa kuwapata wateja.
Soma zaidi: Makontena ya Makonda, siasa za vinyonga nchini
Wateja wachache waliokuwa kwenye mnada huo walionekana kutaja bei lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kufikia kiwango kilichowekwa.
Soma zaidi: Chadema yataka Makonda ajiuzulu