Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Magufuli awazungumzia wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa kutoa rushwa

Video Archive
Fri, 7 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wanakwepa kodi kwa kutoa rushwa na wengine kufanya udalali na kujihusisha na uharifu.

Ametoa kauli hiyo leo Juni 7, 2019  Ikulu jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na wafanyabiashara kutoka Wilaya zote nchini.

Amesema jambo hilo limejitokeza katika biashara ya sukari, mafuta ya kula na korosho.

“Baadhi yao wamekuwa wakitumia mbinu ya kukwepa kodi kwa kudai marejesho ya fedha ya ongezeko la thamani (VAT) wakati mauzo yaliyofanyika ni hewa ya biashara za nje na kwenye hili nataka niseme wazi nina orodha ya kampuni 17,446 ambazo zimehusika na tuhuma hizo,”

 

“Nitawapa copy (nakala) ya kampuni hizo hewa ili mkafanye uchambuzi wenu na kama yalikwepa kitu chochote yakajipange kulipa ndani ya siku 30,” amesema Rais Magufuli.

Habari zinazohusiana na hii

Kiongozi huyo amebainisha kuwa miongoni mwa wanaofanya vitendo hivyo ni waliowahi kubinafsishiwa viwanda na Serikali, kupewa ardhi ili kuviendeleza, kwamba baadhi yao wameamua kuuza mitambo ya viwanda hivyo au kugeuza matumizi ya viwanda bila kufuata utaratibu.

“Wengine wametumia maeneo hayo kukopa fedha benki kwa ajili ya kazi hiyo na hawajafanya, hiyo ni dhambi na wengine najua mko hapa.”

“Baadhi ya wafanyabiashara wamejanga viwanda kama gelesha na kuvitumia kupokea bidhaa kutoka nje bila kulipa kodi stahiki kama vile bidhaa hizo zimetengenezwa nchini.” amesema

Amesema kumekuwa na uongezaji wa marejesho ya fedha ya VAT kwa wafanyabiashara ili waweze kupewa fedha nyingi kutoka serikalini huku akiuita kuwa ni wizi.

Chanzo: mwananchi.co.tz