Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Magufuli apongeza wanafunzi 392 kurudishwa nyumbani, 14 kuchapwa viboko

Video Archive
Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amempongeza mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kuwarudisha nyumbani wanafunzi 392 wa Shule ya Sekondari Kiwanja wilayani Chunya na kuwachapa viboko 14 wanaodaiwa kuchoma moto mabweni mawili ya shule hiyo.

Jana Oktoba 3, 2019 Chalamila aliwachapa viboko  wanafunzi hao kwa madai ya kuhusika kuchoma moto mabweni mawili ya shule yao, leo asubuhi Oktoba 4, 2019 akaagiza wanafunzi 392 kurudi nyumbani hadi Oktoba 28, 2019 wakiwa wamelipa Sh200,000 kila mmoja zitakazotumika kukarabati mabweni hayo.

Wanafunzi 14 waliochapwa viboko wao wametakiwa kutoa Sh500,000 kila mmoja na kuripoti shuleni na wazazi wao huku wengine watano wakiendelea kushikiliwa na polisi kutokana na kutajwa kuhusika moja kwa moja na tukio hilo. Wanafunzi hao wanadaiwa kufanya kitendo hicho baada ya kukutwa na simu 29 kwenye mabweni.

Akizungumza leo katika ziara yake mkoani Songwe, Rais Magufuli amesema viboko vinafundisha na kuwa ipo haja ya kufanyia marekebisho sheria inayozuia adhabu hiyo.

 “Nafikiri kama kuna mahali tulikosea ni ile sheria, inabidi  ikafanyiwe marekebisho wawe wanatandikwa viboko.”

“Eti mkuu wa mkoa anatandika viboko maana yake nini hata Ulaya wanatandika viboko,” amesema Magufuli.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Amesema siku wanafunzi hao wakirejea shuleni lazima wazazi wao walipe fedha hizo kwa ajili ya kukarabati mabweni.

“Na wale wengine (watano) waliohusika kabisa peleka jela. Ndugu zangu nasema haya sio kwamba sina huruma nina upendo mkubwa na nimekuwa mwalimu nafahamu,” amesema Rais Magufuli.

Amesema viboko vinafundisha na vinasaidia kujenga Taifa la watoto wenye nidhamu watakaosaidia kuleta maendeleo.

 “Nimempongeza mkuu wa Mkoa nimempongeza sana, kwa hiyo wakuu wa mikoa fika mahali tandika viboko.”

 “Wewe Silinde ( David- Mbunge wa Momba) shule uliyosoma hukuchapwa viboko? Ulipigwa viboko ndio maana umefika mpaka ubunge. Unaenda pale na simu, ukinyang’anywa simu unachoma jengo? Nidhamu ya namna gani. Hao haki za binadamu wakayajenge basi hayo mabweni,” amesema Rais Magufuli.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz