Pwani. Mkuu mpya wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amemshukuru Rais John Magufuli kwa kumteua na ameahidi kusimamia ilani ya CCM na katiba ya nchi katika utekelezaji wa shughuli zake mbalimbali.
Akizungumza leo Agosti 3 mara baada ya kuapishwa, Jokate amesema si kwamba ana deni kwa Rais tu bali pia kwa vijana wenzake ambao wamekuwa wakimuangalia katika hatua mbalimbali alizopitia.
“Sikuja kutengua torati bali nimekuja Kisarawe kuitimiza kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali waliopo na waliotangulia,”amesema.
Pia amewaomba viongozi wenzake wa Kisarawe kumpa ushirikiano katika utendaji wa kazi ili kufanikisha utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea.
Soma Zaidi:
Magufuli atoa maagizo mazito kwa Ma-RC