Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Gesi yalipuka wanahabari wajeruhiwa

Video Archive
Mon, 16 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Waandishi wa habari wanne wa kampuni za Star Tv, Abood Media, Global Tv na Imani Media wamejeruhiwa na moto baada ya kulipuka kwa mitungi ya gesi kwenye moja ya nyumba mtaa wa Msamvu, manispaa ya Morogoro.

Wanahabari waliojeruhiwa ni Omary Hussein (Star Tv) aliyejeruhiwa mkononi; Hassan Ninga (Imani Media) na  Nicholas Mwanaharusi (Global Tv) waliojeruhiwa kila mmoja mguuni na Salum Yusuf (Abood Media) aliyejeruhiwa usoni, mikononi na miguu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea leo Jumamosi Machi 14, 2020 saa 9:00 alasiri maeneo ya Mafisa katika moja ya nyumba inayohifadhi mitungi ya gesi.

Amesema wanahabari hao walifika eneo la tukio kwa nia ya kuchukua habari baada ya kupata taarifa ya kuungua kwa nyumba hiyo.

Amebainisha kuwa baada ya kurekodi wakiwa wanaondoka eneo hilo, mitungi mingine ililipuka na kuwaunguza. Amesema hali zao zinaendelea vizuri huku mmiliki wa nyumba na muuza gesi wakitafutwa na polisi.

Chanzo: mwananchi.co.tz