Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: CCM yalifungia Gazeti Uhuru

Video Archive
Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Mapinduzi CCM, kimelifungia gazeti la Uhuru leo Agost 11, mara baada ya gazeti hilo kuchapisha sehemu ya mahojiano aliyoyafanya Rais Samia.

Maamuzi haya yamefikiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Daniel Chongolo, huku akionesha kusikitishwa na Taarifa hiyo ya upotoshaji kwa kiongozi mkubwa wa nchi.

Gazeti hilo lilichapisha habari kuu yenye kichwa cha habari "Sina wazo kuwania urais 2025" kauli ambayo waliitoa tofauti na alivyosema rais samia.

Awali CCM walitoa tamko kuhusu chapisho hilo kwa kueleza kuwa watachukua hatua kali za kinidhamu juu ya upotoshwaji huo huku wakilimulika gazeti hilo kama Adamu na Hawa wa magazeti yote nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live