Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Andengenye ahojiwa Takukuru kwa saa nne

Video Archive
Fri, 31 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Aliyekuwa Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye leo Ijumaa Januari 31, 2020 amehitimisha  awamu ya kwanza ya waliokuwa watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Tanzania kuhojiwa na Takukuru.

Mbali na Andengeye, wengine waliohojiwa na taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na rushwa ni aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola na aliyekuwa katibu mkuu, Meja Jenerali Jacob Kingu.

Watakaohojiwa kesho Jumamosi Februari Mosi, 2020 ni naibu katibu mkuu wa wizara hiyo, Ramadhani Kailima na naibu waziri, Hamad Masauni.

Andengenye alifika katika ofisi za taasisi hiyo saa 7:47 mchana na kutoka saa 12:47 jioni.

Wamehojiwa kutokana na agizo lililotolewa na Rasi John Magufuli kutokana na madai  kuwa wamehusika katika mkataba wenye harufu ya ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni.

Andengenye aliondoka eneo hilo akiwa ameshika begi jeusi na kwenda kupanda gari aina ya Land Rover.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Wakati Andengenye akihojiwa kwa muda huo, Lugola amehojiwa kwa saa 5 na dakika 11.

Chanzo: mwananchi.co.tz