Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umuhumu wa kunawa mikono na maji safi na sabuni

288 DSC00587 TZW

Sun, 17 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Asilimia kubwa ya magonjwa ya kuambukiza  hutokana na kutosafisha mikono yetu kabla na baada ya kula au kutoka chooni.

Kutonawa mikono vizuri kwa maji salama na sabuni kunaweza kukakuleta madhara kama  ya kuhara. Baadhi ya watu hawapendalei kunawa mikono yao na maji safi na salama yanayotiririka wakitoka chooni, hali hii imekuwa ikitokea na husababisha waweze kupata magonjwa lama ya kuarisha.

Usipo nawa mikono  vuzuri unazoa vijidudu na kwenda navyo sehemu nyingine kama vile ukimpa mtu mkono unamuachia vijidudu vichafu ama ukienda kula pia unaamisha vijidudu hivyo katika chakula na unavila.

Wataalamu wa masua ya afya wanasisitiza ni wajibu kwa kila mmoja kunawa mikono yake kwa maji safi na salama kabla na baada ili kuuwa vijidudu hivyo na pia kila utakapo chooni hakikisha unanawa na kujifuta vizuri mikono yako na kitambaa chako maalumu, ambacho kitakuwa kinafuliwa kwa usafu mara kwa mara. Ukifanya hivyo unaweza kuepusha maradhi ya tumbo mara kwa mara ambnayo yangeweza kukugharimu hata uhai wako.

Chanzo: bongo5.com