Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy Mwalimu azungumzia mchango wa Mengi sekta ya afya

55638 Pic+ummy

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kifo cha mwenyekiti mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi ni pigo, akitolea mfano jinsi mfanyabiashara huyo maarufu alivyotoa mchango mkubwa katika sekta ya afya kujenga kiwanda cha dawa.

Ummy ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Mei 4 muda mfupi  baada ya kusaini kitabu cha maombelezo nyumbani kwa marehemu Mengi Kinondoni Dar es Salaam.

Mengi  alikutwa na mauti usiku wa kuamkia Mei 2  akiwa Dubai, Falme za Kiarabu.

Waziri huyo amesema amefanya kazi kwa karibu na Mengi tangu alipokuwa naibu waziri, alisaidiana naye kuratibu na kutatua changamoto za walemavu.

“Tumepoteza mtu muhimu alikuwa na mchango mkubwa kutokana na kuwa na dhamira ya dhati ya kuanzisha kiwanda cha dawa hapa nchini,” amesema Ummy.

Amesema pengo lake ni vigumu kuzibika na kwamba  atahakikisha kiwanda cha dawa alichokianzisha kinakamilika.



Chanzo: mwananchi.co.tz