Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy Mwalimu; Waziri aliyedumu miaka 14 baraza la mawaziri

Watanzania Tujenge Utamaduni Wa Kupima Afya   Ummy.jpeg Ummy Mwalimu; Waziri aliyedumu miaka 14 baraza la mawaziri

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa Agosti 14, 2024 unaweza usisahaulike haraka katika maisha ya kisiasa ya Ummy Mwalimu.

Hii inatokana na uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumweka kando katika mabadiliko madogo aliyoyafanya katika Baraza lake la Mawaziri.

Ummy ambaye ni Mbunge wa Tanga Mjini (CCM) ni miongoni mwa mawaziri wachache waliodumu katika Baraza la Mawaziri kama wawaziri kamili kwa takribani miaka tisa mfululizo. Alihama kutoka hapa kwenda pale.

Ukijumuisha miaka tisa ya uwaziri na miaka mitano ya naibu waziri kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, Ummy anakuwa na miaka 14 ndani ya baraza la mawaziri akihudumu katika tawala tatu. Ya Jakaya Kikwete, John Magufuli na sasa ya Samia Suluhu Hassan.

Ummy amekuwa mmoja wa mawaziri waliohudumu Wizara ya Afya kwa kipindi kirefu na ndani ya utawala wa awamu ya tano ulioingia madarakani Novemba 5, 2015 ulipounda Serikali Desemba mwaka huo hadi ulipokoma Machi 17, 2021 alikuwa wizara hiyo.

Huo ulikuwa utawala wa Rais John Magufuli ambaye alifariki dunia Machi 17, 2021 na nafasi yake kushikwa na Samia ambaye wakati huo alikuwa Makamu wa Rais.

Katika utawala wa Magufuli, Ummy ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alikuwa miongoni mwa mawaziri sita ambao hawakuwa wanaguswa kwenye panga pangua.

Wengine ambao hawakuguswa na wizara zao kwenye mabano ni, Jenista Mhagama (Sera, Bunge, Uratibu), Profesa Joyce Ndalichako (Elimu), William Lukuvi (ardhi) na Dk Philip Mpango (Fedha na Mipango) na Dk Hussein Mwinyi wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kwa sasa Dk Mpango ni Makamu wa Rais wa Tanzania na Dk Mwinyi ni Rais wa Zanzibar.

Ummy aliyezaliwa Septemba 5, 1973 alikuwa sehemu ya baraza la kwanza la Magufuli alilolitangaza Desemba 10, 2015 alipoteuliwa kuwa Waziri wa Afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live