Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukikutwa na silaha ya aliyefariki, jela miaka 15 - VIDEO

Video Archive
Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Tanzania limewataka Wananchi kusalimisha silaha zilizokuwa zinamilikiwa kihalali na Ndugu zao ambao kwa sasa ni Marehemu, ili silaha hizo zisilete madhara katika Jamii na kusema kuendelea kuhifadhi silaha hizo nyumbani ni kinyume cha sheria na atakayepatikana akimiliki silaha hizo akikurwa na hatia Mahakamani anaweza kufungwa miaka 15 jela au faini ya Tsh. milioni 10 au vyote kwa pamoja.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Polisi, David Misime leo June 28,2024, imesema “Kwa mujibu wa kifungu cha 55 cha Sheria ya Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015 ni kwamba Mmiliki wa silaha mara anapofariki, Ndugu wa Marehemu wanapaswa kuisalimisha silaha hiyo katika kituo cha Polisi kilicho karibu wakati taratibu za mirathi na umilikishwaji kwa Mtu mwingine kwa mujibu wa sheria zikiendelea”

“Watambue kuwa kuendelea kuhifadhi silaha hizo nyumbani ni kinyume cha sheria na yeyote atakayepatikana akimiliki silaha hizo atakuwa ametenda kosa na endapo akipatikana na hatia Mahakamani, anaweza akapewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka kumi na tano jela au faini ya shilingi milioni kumi au vyote kwa pamoja”

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limesema limebaini kuwepo kwa baadhi ya kampuni binafsi za ulinzi ambazo zinamiliki silaha aina ya Gobore bila kuwa na vibali kinyume na utaratibu wa sheria unaozitaka kampuni za ulinzi kumiliki shotgun kwa ajili ya shughuli za ulinzi.

“Kutokana na hilo, wamiliki wa kampuni binafsi za ulinzi wanafahamishwa kuwa ni marufuku kutumia silaha aina ya Gobore kwa kazi za Ulinzi na wanaofanya hivyo wanaelekezwa kuacha mara moja kwani ni kinyume cha sheria, Wamiliki hao wanashauriwa kufuata utaratibu wa kisheria wa kumiliki silaha aina ya Shotgun kwani ndizo zinazoruhusia kutumika kwa shughuli za ulinzi, Jeshi la Polisi linatoa muda wa miezi miwili kuanzia tarehe 1/7/2024 hadi 31/8/2024 na baada ya kipindi hicho kutakuwa na msako mkali ambapo Kampuni binafsi ya ulinzi itakayokutwa ikimiliki silaha hizo itachukulia hatua za kisheria”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live