Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukali wa Waitara kwa waliosema ujenzi umekwama Kimara-Kibaha (video+)

Video Archive
Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: millardayo.com

Serikali imewataka waandishi wa habari nchini kuzingatia misingi ya taaluma ya uandishi wa habari pindi wanapotekeleza majukumu yao pasipo kuleta taharuki kwa jamii na Taifa.

Aidha waandishi hao wameaswa kupata taarifa sahihi hasa za miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na Serikali kupitia vyanzo sahihi.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, ameyasema hayo leo wakati akikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa barabara ya Morogoro (Kimara – Kibaha) km 19.2 kuwa njia nane ambao ujenzi wake umefikia asilimia 94 na kubakiza kazi ndogondogo ambazo zinatarajiwa kumalizika  mwisho wa mwezi Disemba, 2021.

Chanzo: millardayo.com