Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukaguzi vyombo vya moto marufuku kutoa 'cash'

Ukaguzi Gari Basi Ukaguzi vyombo vya moto marufuku kutoa 'cash'

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Nchini limesema kuwa kila mwaka huadhimisha wiki ya nenda kwa usalama barabarani huku likipiga marufuku kwa Mtu yoyote kupokea ama kutoa fedha taslimu wakati wa ukaguzi wa vyombo vya moto.

Akiongea jana Julai 21, 2024 Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, DCP David Misime amesema kuwa kipindi cha kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto Wamiliki waelekezwe kurekebisha kasoro zilizobainika au kuondoa chombo husika kwa matumizi ya usafiri kama kitabainika kuwa na ubovu mkubwa na kusema ukaguzi unafanyika kulingana na sheria na kanuni za usalama barabarani zinavyoelekeza.

Amesema ukaguzi unaofanyika kwa mwaka huu, Mmiliki wa chombo cha moto atalipa ada ya ukaguzi kupitia namba ya malipo (control number) atakayopewa au atakayopakuwa kutoka katika mfumo ndipo chombo chake kitakaguliwa na kupatiwa stika na kusisitiza katika ukaguzi unaoendelea hakuna fedha taslimu itakayopokelewa mkononi ama na Askari, Afisa wa Polisi au wanaojifanya vishoka.

“Fedha yeyote kwa ajili ya ukaguzi wa chombo cha moto ilipwe kupitia mfumo wa malipo ya Serikali kwa kutumia namba ya malipo (control number), atakayebainika kutoa malipo ya fedha ya ukaguzi wa chombo cha moto mkononi (cash) au atakayepokea malipo hayo mkononi awe Mmiliki, Askari,kishoka au yeyote yule atakamatwa na kufikishwa Mahakamani.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live