Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UCHAGUZI AFRIKA KUSINI: nani kumrithi Jacobo Zuma?

256 Zuma TZW

Sat, 16 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Mkutano Mkuu wa 54 wa chama tawala nchini Afrika kusini cha African National Congress (ANC) unafanyika huku agenda kubwa ikiwa ni nani atarithi uongozi wa chama cha ANC kutoka kwa Rais Jacob Zuma.

Rais Zuma ambaye aliingia madarakani akimrithi Thabo Mbeki, amekuwa akiandamwa na kashfa za ufisadi kwa muda mwingi wa uongozi wake, kumekuwa na jitihada za kumvua madaraka na kumburuza mahakamani ambazo zimekuwa zikigonga mwamba.

Kinyanganyiro hiki cha uongozi kinakutanisha watu sita ingawa ni wawili wenye kupewa nafasi kubwa.

Wa kwanza ni mke wa zamani wa Rais Zuma, Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye pia amewahi kuwa kiongozi wa AU, wa pili ni Makamu wa rais  wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa  ambaye ni mmoja wa matajiri wakubwa Nchini Africa ya kusini.

Pamoja na kujikwamua kutoka kwenye ubaguzi, wengi wa wananchi wa Afrika ya kusini bado wanaishi kwenye maisha duni huku Nchi hiyo ikiwa ni moja ya Nchi zenye utajiri mkubwa wa maliasili na uchumi mkubwa barani Afrika.

FAMILIA YA LISSU TENA, KUHUSU MAMA SAMIA KWENDA NAIROBI NA MENGINE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com