Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tutatekeleza ahadi alizoahidi Kwandikwa - Majaliwa

Majaliwa Web Tutatekeleza ahadi alizoahidi Kwandikwa - Majaliwa

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali itatekeleza na kuenzi mipango yote ikiwemo ahadi zote zilitolewa kwa wana Ushetu na aliyekuwa mbunge na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Jenga Taifa, marehemu Elias Kwandikwa. 

Waziri Mkuu amesema hayo leo Jumatatu Agosti 9, 2021, alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, katika mazishi ya marehemu Kwandikwa kijijini kwao Butibu, Ushetu, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.

"Tumepoteza kiongozi aliyekuwa anaongoza majeshi yetu, amefanya kazi nzuri sana katika kipindi chote cha uhai wake alipokuwa anaitumikia serikali, marehemu alikuwa mwadilifu, mwajibikaji na aliyefanya kazi kwa weledi mkubwa," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Marehemu Waziri Elias Kwandikwa, alizaliwa Julai 7, 1966 wilayani Kahama, Shinyanga na alifariki dunia Agosti 2, 2021 katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Chanzo: eatv.tv