Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu katika kampeni zake zilizofanyika katika Mji wa Makambako amesema Serikali ya chama hicho ikiingia madarakani itaondoa utitiri wa kodi na kuzuia ukandamizwaji wa wafanyabiashara.
Lissu amesema hayo wakati akinadi sera zake na kuahidi kuwa, atahakikisha wafanyabiashara ambao kweli wana madeni wanawekewa utaratibu mzuri wa kulipa ili wasiathiri biashara zao, lakini pia amesema ataboresha mahusiano ya Kimataifa yenye kuleta tija katika uchumi.
“Kuwa na deni sio ishu, kama unanilazimisha nilipe deni ili watoto walale njaa kwa sababu tu ya deni hiyo sio sawasawa, kama unataka nilipe deni ili biashara yangu ife hiyo sio sawasawa” Lissu
“Kwa hivyo tunaweka utaratibu kwa wafanyabiashara wenye madeni wataweza kulipa madeni yao bila kuua biashara zao” Lissu
CHADEMA WAIANGUKIA TUME “TUMEIANDIKIA BARUA KUHUSU RUFAA ZA UBUNGE NA MADIWANI”