Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tundu Lissu afuata gari lake Polisi lililoshambuliwa Septermber 7, 2017

Maxresdefault 1 4 660x400 Tundu Lissu afuata gari lake Polisi lililoshambuliwa Septermber 7, 2017

Thu, 27 Aug 2020 Chanzo: millardayo.com

Mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu ametembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuchukua gari lake ambalo limehifadhiwa na Jeshi la Polisi Mkoa huo jaribio la mauaji dhidi ya Lissu la tarehe 7 September 2017.

Lissu ameambatana na mgombea mwenza wake Salum Mwalimu na alipokelewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Giles Muroto.

Katika mazungumzo yake na SACP Muroto, Lissu amesema kwamba ameamua kuja yeye mwenyewe baada ya utaratibu wa kulipata hilo kwa njia zingine kushindikana.

Kwa upande wake, SACP Muroto alimweleza Lissu kwamba Jeshi la Polisi mkoani hapo linahitaji muda zaidi ili kujiandaa kulikabidhi gari hilo kwake.

Aidha, SACP Muroto alimweleza Lissu kwamba Jeshi la Polisi linamhitaji atoe maelezo kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwake September 2017.

Lissu alijibu kwamba yeye yuko tayari kutoa maelezo polisi kwa tarehe na muda utakaokuwa muafaka kwa pande zote mbili.

Lissu alisisitiza mshangao wake kwamba hadi sasa, takriban miaka mitatu tangu kushambuliwa kwake, Jeshi la Polisi halijafanya uchunguzi wowote, ikiwemo kumhoji yeye na dereva wake Adam Bakari Mohamed, licha ya kuahidi kwamba lingefanya tangu Lissu akiwa hospitalini nchini Kenya.

DC ARUSHA AIMBA HIPHOP JUKWAANI, WANANCHI WASHANGILIA

Chanzo: millardayo.com