Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tulia ataka wafanyakazi wa kujitolea wapewe kipaumbele katika ajira

Tulia Ackson Dp Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameiagiza Serikali kuja na utaratibu maalumu kwa wanaofanya kazi za kujitolea kabla ya kuwa na sheria ya kuwasaidia kupata ajira bila kikwazo zinapotolea.

Spika ametoa mapendekezo hayo leo Jumatatu Septemba 4, 2023 wakati wabunge wengi walipouliza kuhusu nafasi ya watu wanaojitolea kutopata kipaumbele kwenye ajira mpya.

“Mheshimiwa Waziri, pamoja na kuwa hamjaleta sheria lakini ni vyema mkaangalia na kuwepa mpango maalumu kwa wanaofanya kazi za kujitolea ili inapotokea nafasi za ajira wapate moja kwa moja,” amesema Dk Tulia.

Katika swali la msingi Mbunge wa Kiteto (CCM), Edward Olelekaita alihoji ni lini Serikali itapeleka bungeni marekebisho ya Sheria ya Ajira ya Utumishi wa Umma kuongeza kigezo cha kujitolea ili kutoa fursa kwa wanaojitolea.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ridhiwan Kikwete amesema amesema kwa sasa Serikali inafanya mapitio ya Sheria ya Utumishi wa Umma sura 298, sera ya menejimenti na ajira katika utumishi wa umma.

Amesema lengo ni kuhakikisha Serikali inaongozwa na utaalamu na weledi “meritocracy” na usawa wa fursa za ajira kwa Watanzania wote.

Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene amesema Serikali haitakuwa tayari kuona mtumishi anayehitajika akibaki mtaani wakati kuna upungufu.

“Haipendezi kuona daktari akilima matikiti wakati sisi tunauhitaji wa madaktari au walimu kuzagaa mtaani wakati wamesomeshwa kwa rasilimali za nchi, tunakuja na mpango mkakati wa kumaliza tatizo hilo,” amesema Simbachawene.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: