Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuhuma zinazomkabiri Boniface Jacob zaanikwa, kilichokutwa ndani mwake...!

Polisi Walivyomkamata Na Kumpekua Boniface Jacob Nyumbani Kwake.png Boniface Jacob

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi wamemaliza kufanya upekuzi nyumbani kwa Meya wa zamani wa Ubungo ambaye pia ni Kada wa CHADEMA, Boniface Jacob ambaye amekamatwa na Polisi akiwa maeneo ya Sinza na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar es salaam jana jioni September 18, 2024 kisha baadaye kwenda nae nyumbani kwake Msakuzi Jijini Dares Salaam.

Upekuzi umeanza saa tatu kasoro usiku na kumalizika saa sita kasoro usiku huu ambapo kwa sasa Boniface anarejeshwa tena Oysterbay.

Kwa mujibu wa Wakili wa Boniface Jacob, Hekima Mwasipu, Boni anatuhumiwa kwa kusambaza taarifa za uongo.

Katika mazungumzo yake, Mwasipu alieleza kwamba polisi walikuwa makini katika upekuzi wao, ambapo walizingatia maeneo maalum ndani ya nyumba ya Jacob. "Polisi wamechukua nyaraka fulani aliyokuwa akiandika Boniface Jacob, ambazo zinaonekana kuwa mukhtasari wa shughuli zake za kisiasa. Baada ya kuzipata, waliamua kuondoka nazo bila kutoa maelezo zaidi," alisema Wakili Mwasifu.

Wafuasi wa CHADEMA pamoja na majirani wa Jacob walikuwa na wasiwasi kuhusu kilichokuwa kinaendelea ndani ya nyumba hiyo, huku wengi wakihofia kuwa polisi walikuwa na lengo la kumchafua Jacob kwa mashtaka yasiyo wazi. Video na picha za upekuzi huo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, zikiibua mijadala mikali juu ya hatua hiyo ya vyombo vya usalama.

Licha ya upekuzi huo, bado Jeshi la Polisi halijatoa maelezo ya kina kuhusu sababu za kumkamata Boniface Jacob, huku uvumi na tetesi zikiendelea kusambaa. Wakili Mwasifu amesisitiza kuwa timu ya mawakili wa CHADEMA iko tayari kupambana kisheria kuhakikisha haki inatendeka na Jacob anapatiwa haki zake zote.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ametoa taarifa jioni jana akikiri Polisi kumshikilia Boniface kutokana na makosa ya kijinai anayotuhumiwa nayo “Wananchi wapuuze uongo unaosambazwa mitandaoni kuwa ametekwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live