Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trafiki washambuliwa, wajeruhiwa, 2 wakamatwa

Trafiki Serengeti Trafiki washambuliwa, wajeruhiwa, 2 wakamatwa

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 15 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwashambulia askari wawili wa kikosi cha usalama barabarani waliokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi katika eneo la Natta wilaya ya Serengeti.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake David Misime inasema kuwa

“Tarehe 18/09/2024 majira ya saa 12:00, Kijiji cha Natta katika barabara ya Bunda Mugumu, askari Polisi koplo Peter akiwa na koplo Paulo wakiwa katika majukumu yao ya kikazi walisimamisha gari la abiria lenye namba T 476 ECP aina ya TATA lililokuwa likitokea mkoani Mwanza kwenda Serengeti mali ya Kampuni ya Jimmy safari likiendeshwa na Haruna January Ally.

Baada ya gari hilo kusimama walianza ukaguzi wa gari hilo na ndipo askari hao waliingia ndani ya gari kwa ajili ya ukaguzi wa gari hilo lililokuwa limezidisha abiria wakati wakiendelea na majukumu yao dereva aliondoa gari hilo huku kondakta na utingo na baadhi ya abiria walianza kuwashambulia askari hao kwa kuwapiga sehemu mbalimba za mwili kitendo kilicho pelekea Koplo Paulo kujeruhiwa vibaya jicho la kulia. Watuhumiwa wote kumi na tano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa upelelezi zaidi na mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya mwendesha mashitaka kwa hatua zaidi.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa watu wenye tabia za kujichukulia sheria mkononi na kwamba halita mvumilia mtu yeyote mwenye tabia kama hizi na hatua kali za kisheria zitachukuliwa” David Misime

Chanzo: www.tanzaniaweb.live