Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tarimba ataka wanaume kupewa mikopo ya halmashauri

Tarimba Picee Tarimba ataka wanaume kupewa mikopo ya halmashauri

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba amehoji ni kwa nini Serikali isiongeze kundi la wanaume katika mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.

Tarimba alihoji ni kwa nini Serikali isiongeze kundi la wanaume kwa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Deogratius Ndejembi amesema mikopo ya asilimia 10 inatolewa kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290 Kifungu cha 37A ya Mwaka 2018 na Kanuni za Usimamizi na Utoaji wa Mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu za Mwaka 2019 na Kanuni za Marekebisho za Mwaka 2021.

Amesema mikopo ya asilimia 10 inatolewa kwa ajili ya kuwezesha makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupata mikopo isiyo na riba kwa kuzingatia kwamba makundi haya hayawezi kupata mikopo katika taasisi zingine za fedha kwa sababu ya kukosa dhamana na uwezo mdogo wa kumudu riba ili waweze kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: