Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzia: Kifo cha Dk. Mwele Malecela, Viongozi Wamlilia

Dk Malecelaaaa Tanzia: Kifo cha Dk. Mwele Malecela, Viongozi Wamlilia

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KUFUATIA kifo cha Dkt. Mwele Ntuli Malecela ambaye amefariki dunia, leo Alhamisi, Februari 10, 2022, Geneva mchini Uswisi, viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali wameshindwa kujizuia na kueleza masikitiko yao kufuatia msiba huo.

Balozi Hoyce Temu; Ofisi ya Uwakilishi @UbaloziGeneva imepokea kwa masikitiko makubwa sana kifo cha Mtanzania mahiri na mchapakazi wa kitaifa na kimataifa #drmwele kilichotokea Leo hapa #Geneva #Uswisi. Pole sana kwa Familia na Watanzania wote hasa wanafamilia wa Geneva. #RIP

Mbunge Dk. Faustine Ndugulile; I am saddened by the death of Dr @mwelentuli earlier today. She was a sister, friend and confidant. Mwele was always on top of things. She played a critical role in my first Parliamentary campaign in 2010. I'll remember her for her kindness. May her soul rest in eternal peace.

DC Jokate Mwegelo; Rest In Peace Dr. Mwele

MBUNGE DITOPILE

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Dkt. Mwele Malecela aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI) pia alikua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) alikua Mkurugenzi wa Udhibiti wa Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele"

Maria Sarungi Tsehai; Broken heart I am absolutely floored! And still can’t believe it! Mwele! Loudly crying face. You accomplished many great things that some of us can only dream of. You worked hard and always followed the path of honesty. May God grant you a beautiful and peaceful eternal rest! Love and prayers to family.

Mwele Ntuli Malecela alizaliwa tarehe 26 Machi 1963, alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI). Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela alikua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo alikua Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live