Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taarifa ya hesabu za CAG kuanza kuchambuliwa leo

BUNGE LA 12 MKUTANO WA 11 Taarifa ya hesabu za CAG kuanza kuchambuliwa leo

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchambuzi wa Taarifa za Hesabu zilizokaguliwa na CAG kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Juni 30, 2022 ni miongoni mwa shughuli za kamati za kudumu za bunge zitakazofanywa na vikao vya kawaida vya kamati hizo vitakavyoanza Jumatatu Agosti 14-25, 2023 Jijini Dodoma.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Bunge jana Jumapili, Agosti 6, 2023 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa inasema Kamati tano zitatangulia kuanza vikao, ambapo nne kati ya hizo zitaanza vikao Agosti 7, 2023 na Kamati moja ya Bajeti itaanza Agosti 10, 2023 ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 12 wa Bunge utakaoanza Agosti 29, 2023.

Maeneo yatayoshughulikiwa ni yenye matumizi mabaya ya fedha za umma. Shughuli hii itatekelezwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kwa mujibu wa Kifungu cha 13, Kifungu cha 14 na Kifungu cha 15 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023.

Shughuli nyingine zitakofanywa na kamati katika kipindi hicho zitakuwa ni uchambuzi wa Miswada miwili (2) ya Sheria utakaofanywa na Kamati mbili ambazo ni Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria na Kamati ya Bajeti.

Shughuli nyingine ni uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa wakati wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge, uchambuzi wa Taarifa za Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa lengo la kuliwezesha Bunge kufuatilia ufanisi na tija kwa Mitaji ya Serikali kwenye mashirika mbalimbali na taasisi na Uchambuzi wa Taarifa za Utendaji za Wizara kwa lengo la kuliwezesha Bunge kutekeleza jukumu la kuisimamia na kuishauri Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: