Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Mama mzazi wa wa Halima Mdee afariki Dunia(+Video)

Video Archive
Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama Mzazi wa Mbunge wa viti Maalum wa CHADEMA, Halima James Mdee Bi.Theresia Mdee, amefariki Dunia leo Julai 30, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Mbunge, Ester Bulaya, ambaye ni rafiki wa karibu na Halima Mdee kabla ya umauti kumfika Bi Theresia alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na alipita hospitali mbalimbali ikiwemo ya Benjamin Mkapa. Pia ameeleza taratibu za mazishi zinaendelea na taarifa itatolewa baadaye kwa undani zaidi.

Itakumbukwa kuwa Februari 1, Mwaka huu Rais Samia akiongozana na baadhi ya viongozi wa Serikali alimtembelea Bi Theresia Mdee akiwa amelazwa Hopitali hapo na kupata wasaa wa kumpa neon la faraja.

Endelea kuwa nasi kwa Tanzaniaweb taarifa Zaidi, Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live