Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAKUKURU yawaburuza mahakamani watumishi 16 Sengerema - Video

Video Archive
Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Mwanza imewafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Sengerema watumishi 16 wa Halmashauri ya Sengerema kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha Zaidi ya Shilingi Zaidi ya milioni 87 zilizotokana na mapato ya ndani.

Akisoma mashtaka yanayowakabili Mwanasheria mwandamizi wa Tasisis ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza Moses Malewo mbele ya Hakimu Mwandamizi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Sengerema Evoid Augen Kisoka amesema kuwa watumishi hao wote wanakabiliwa mashtaka mbalimbali yakiwemo mashtaka ya matumizi mabaya ya Mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kupambana na Rushwa na kifungu cha 28 cha ufujaji na ubadhilifu.

Hata hivyo washitakiwa hao wote baada ya kusomewa mashtaka yao wameachiwa kwa dhamana ambapo baadhi watafikishwa tena mahakamani hapo June 19 na wengine June 25 mwaka huu.

Baada ya kusoma mashtaka hayo Mwanasheria mwandamizi wa Tasisisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza Moses Malewo akiwa nje ya viunga vya mahakama amezungumza na waandishi wa habari na kuwatahadharisha watumishi wa Halmshauri kuzingatia sheria kanuni na sheria zinazowaongoza katika ukusanyaji wa mapato na kutojihusisha na vitendo vya rushwa .

Sauti ya mwanasheria mwandamizi wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Moses Malewo akizungumzia watuhumiwa wa ubadhilifu wa fedha zaidi ya mil.87 Sengerema Nao baadhi ya wananachi Wilayani Sengerema wameipongeza Takukuru kwa kuwafikisha mahakamani watumishi hao huku wakiomba kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wale watakaobainika kujihusisha na ubadhilifu huo wa fedha kwa kuwa wanachangia kurudisha nyuma maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live