Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Studio za Mjini FM Radio zateketea kwa moto

Mjini FM72 Studio za Mjini FM Radio zateketea kwa moto

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Studio ya kurushia matangazo ya Kituo cha Radio cha Mjini FM kilichopo Jijini Dar es salaam imeteketea kwa moto jana Januari 12,2024 huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.

Akiongea baada ya kufika eneo la tukio Insp. Kulwa Nzelekela kutoka Jeshi la Zimamto na Uokoaji amenukuliwa akisema walipata taarifa saa moja na dk 15 asubuhi leo na wakafanikiwa kufika eneo la tukio saa 1 na dk 27 asubuhi na kuanza kupanbana na moto huo ambao tayari ulikuwa umeshika kasi na kupelekea studio ya Mjini FM eneo lote kuteketea kwa moto.

“Kuna baadhi ya vitu vimeokolewa lakini inawezekana vimeathirika kwa moto lakini studio yote imeteketea kwa moto, jengo lipo salama sehemu iliyoathirika ni sehemu ya studio pekee yake, saa 12 asubuhi studio ilianza kazi, waliokuwepo wamesema waliona moto umeanzia juu ya dari ukadondoka kwenye meza zao za studio na moto

Tanzaniaweb.com inatoa pole nyingi kwa Wenzetu wa @MjiniFM katika kipindi hiki kigumu, tunawaombea wepesi katika kuijenga upya studio yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live