Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbachawene azungumzia video ya waliovua nguo ukumbini, taa kuzimwa

Simba Chawenepiccc Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema wameutambua ukumbi lilikotokea tukio la mwanamke na mwanaume kuvua nguo hadharani na baadhi ya watu wamekamatwa na wengine wanatafutwa.

Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakiwa katika ukumbi huo huku mtu mmoja akitangaza kuwa wahusika ambao ni mwanamke na mwanaume watavua nguo jambo ambalo lilitekelezwa na wawili hao kisha taa zikazimkwa huku baadhi ya watu ukumbini hapo wakitumia simu kurekodi tukio hilo.

“Vueni nguo kisha mtakutana katikati kitakachotokea mimi sijui,” amesikika akisema mshereheshaji wa shughuli hiyo huku wawili hao wakiwa watupu wakisakata muziki na kusogeleana na kisha kukumbatiana.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 16, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari, Simbachawene amesema kwa sasa hawezi kueleza idadi ya waliokamatwa wala majina yao kwa kuwa upelelezi unaendelea.

Chanzo: Mwananchi