Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbachawene awataka watumishi Mambo ya Ndani kuwa wazalendo

7c209b682cf4bef421ce4067875db96b.jpeg Simbachawene awataka watumishi Mambo ya Ndani kuwa wazalendo

Sat, 12 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutokubali kutumika na kuwa wazalendo kwa nchi ili kukuza amani na usalama.

Alisema hayo jana mjini hapa wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Ndani cha kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu hadi kufikia robo ya pili ya mwaka 2020/2021.

Simbachawene alisema kila moja anatakiwa kuwa mzalendo kwa kulinda amani na usalama wa nchi na wasikubali kutumika bali wauvae uzalendo kwa ajili ya nchi yao.

“Jeshi la polisi ,uhamiaji ni kiungo cha usalama wa nchi kama hawajatekeleza wajibu wao vizuri yote yaliyofanyika yanaweza kuharibika kwa pamoja.. msikubali kutumika mnatakiwa kuwa wazalendo kwa nchi yenu,” alisema.

Simbachawene alisema baraza la wafanyakazi si kwa ajili ya kudai haki tu bali ni pamoja na kutimiza wajibu.

Alisema serikali tangu mwaka wa fedha 2020/2021 uanze kumekuwa na mtiririko mzuri wa fedha kutoka hazina hali ambayo imesaidia watumishi kuanza kupata stahili zao hususani malipo ya likizo na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za wizara.

Aidha alisema vyombo vya ulinzi na usalama viliweza kusimamia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 vizuri kwa weledi na kuwa uchaguzi huo ulidhihirisha namna watanzania walivyokomaa katika demokrasia za vyama vingi na wameudhihirishia ulimwengu kwa vitendo.

“Natumaini kila mmoja ameelewa vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na hotuba ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na maelekezo yake yote kila mmoja akatimize wajibu wake ili kuweza kumsaidia Rais katika kuleta maendeleo ya wananchi,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz