Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbachawene awashukia waharibifu wa mazingira

Waziri Simbachawene: Rushwa Ndogondogo Zinakera Sana Wananchi Simbachawene awashukia waharibifu wa mazingira

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene amesema kukatika kwa daraja la Kidunda, kumetokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mengi, huku akiwashukia wananchi wanaoharibu mazingira kwa kulima na kukata miti maeneo ya milimani kuwa chanzo cha tatizo hilo.

Simbachawene ametoa kauli hiyo jana Februari 4, 2023 wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Kibakwe, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo daraja hilo linalounganisha upande wa Kusini mwa Jimbo la Kibakwe, ni muhimu kwa wakazi wa meneo hayo kwani hutumiwa kwa ajili ya shughuli za usafiri kwa wananchi wote wanaokwenda katika wilaya ya Mpwapwa.

"Nawashuukuru sana Tarura Mpwapwa na Tanroads mkoa wa Dodoma kwa utayari wao tangu Januari 31, 2024 daraja hili lilipokatika walifika kuhakikisha utengenezaji wa daraja mpya linaanza mara moja," amesema Simbachawene.

Pia, ameagiza viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi wilaya pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuhahakisha hakuna wananchi wanaokata miti na wala kulima juu ya milima.

Diwani wa Kibakwe David Chisanza amesema changamoto ya uharibifu wa mazingira ndio sababu iliyochangia daraja kukatika, akisema kuna watu wamekamatwa na wamepelekwa Mpwapwa lakini kesi zao zimekuwa zikiishia juu kwa juu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live