Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu George Simbachawene, amempongeza Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Iramba Yasinta Chipanjile, kwa kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba.
Kauli hiyo ameitoa katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kata ya Rudi jimbo la Kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa ambapo alifanya mkutano wa hadhara na kutembelea mradi wa maji.
"Ameweza kufaulisha wanafunzi 32 kati ya wanafunzi 40 baada ya kuwaahidi kwenda Bungeni mjini Dodoma, wanafunzi hao wamefaulu kwa wastani wa daraja B na Daraja C, watoto wana akili sana ila wazazi wao wanawaambia wasifaulu kwa sababu hawana fedha ya kuwasomesha, hivyo mvuruge mvuruge majibu ili msifaulu,," amesema Waziri Simbachawene
"Nchi hii inataka watu wasomi, mwezi wa kwanza nitawapeleka bungeni Mjini Dodoma serikali ya chama cha mapinduzi inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetangaza elimu bure ya msingi na sekondari hakuna ada," ameongeza Waziri Simbachawene
Naye Mwalimu Yasinta Chipanjile wa shule ya Msingi Iramba amesema amepata changamoto katika kipindi cha miaka miwili kutokana na kushindwa kucheza na akili za wazazi.