Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbachawene achukua mikoba ya Hawa Ghasia

14363 Pic+simba+chawene TanzaniaWeb

Tue, 28 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya bajeti leo Jumanne Agosti 28, 2018.

Katika uchaguzi huo, mbunge wa Maswa Magharibi (CCM), Mashimba Ndaki amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.

Uchaguzi wa viongozi wa kamati hiyo umefanyika baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, Hawa Ghasia na makamu wake, Jitu Soni.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, Simbachawene amesema mapema leo alihamishwa kutoka kamati ya Bunge ya katiba na sheria kwenda kamati ya bajeti.

Amesema baada ya kuhamishwa na kukuta nafasi  ipo wazi, aliamua kugombea uenyekiti na kushinda kwa kishindo.

Chanzo: mwananchi.co.tz